Jawabu kutoka kwa baadhi ya wanazuoni wetu ni kama ifuatavyo:
Ofisi ya kielimu ya Ayatu-Llahi Khamenei (Mungu amhifadhi) yenye kuhusika na kujibu maswali ya kifiqi, imetoa jawabu ifuatayo:
Iwapo mwanamke alimuakilisha mwanamme huyo kuisoma na kuinuia ndoa, pamoja na kumpa yeye uwakili wa kuainisha mahari pamoja na muda wa ndoa hiyo, ndoa hiyo haitakuwa na matatizo, lakini tu kinachotakiwa kuzingatiwa ni kwamba: ni wajibu kuchukua tahadhari katika kuifunga ndoa hiyo, yaani kunatakiwa zizingatiwe sharti za ndoa, na miongoni mwa sharti hizo, ni kutaka ruhusa kutoka kwa walii wa mwanamke, iwapo mwanamke huyo atakuwa ni bikra.
Ofisi ya kielimu ya Ayatu-Llahi Sistani (Mungu amhifadhi) yenye kuhusika na kujibu maswali ya kifiqi, imetoa jawabu ifuatayo:
Ndoa hiyo haina matatizo na imesihi.
Ofisi ya kielimu ya Ayatu-Llahi Makaarim Shirazi (Mungu amhifadhi) yenye kuhusika na kujibu maswali ya kifiqi, imetoa jawabu ifuatayo:
Iwapo mwanamme huyo alipewa unaibu wa kuifunga ndoa pamoja na unaibu wa kuainisha muda na mahari, basi ndoa yao itakuwa imesihi na haina mashaka.
Ofisi ya kielimu ya Ayatu-Llahi Safi Gulpegani (Mungu amhifadhi) yenye kuhusika na kujibu maswali ya kifiqi, imetoa jawabu hii:
Iwapo mwanamme atakuwa ameifunga ndoa hiyo kwa nia ya muda maalumu na mahari maalumu, lakini mwanamke akawa hana habari juu ya hilo, kisha mwamke huyo akapata habari baada ya muda fulani kuhusu kiwango cha mahari pamoja na muda halisi wa ndoa hiyo, ndoa yao itasihi.
Ofisi ya kielimu ya Ayatu-Llahi Mahdi Hadawiy Tehraniy (Mungu amhifadhi) yenye kuhusika na kujibu maswali ya kifiqi, imetoa jawabu ifuatayo:
Iwapo wewe (mwanamke) ulimpa huyo mwanamme uwakili wa yote hayo, yaani kuifunga ndoa pamoja na kuainisha muda na mahari, yaani wewe ulimpa mwanamme ruhusa ya kuanisha yeye mwenyewe muda anautaka na mahari anayo yataka. Ndoa yenu itakuwa ni sahihi, lakini iwapo wewe utakuwa hukumpa yeye aina hiyo ya uwakili na unaibu, basi usahihi wa ndoa hiyo utategemea ridhaa yako wewe baada ya wewe kujua na kufahamu kiwango cha mahari na muda wa ndoa alichokianisha mwanamme huyo, kwa hiyo kuridhika na kukubali kwako wewe juu ya hilo, ndiko kutakoifanya ndoa hiyo ipasi na iwe salama.
Kwa ajili ya kunufaika zaidi kuhusiana na masuala ya ndoa ya muda mfupi, angalia maswali yafuatayo katika tuvuti yetu:
1- Swali namba 1238: kuhusiana na masharti ya ndoa za muda mfupi, namba ya swali kwenye tovuti ni 1225.
2- Swali namba 2190: kuhusiana na ndoa ya muda mfupi kwa aliyekuwa bikra, namba ya swali katika tovuti ni 2315.
2- Swali namba 3237: kuhusiana na ulipaji wa mahari ya ndoa ya muda mfupi, namba ya swali katika tovuti ni 3494.
4- Swali namba 7454: kuhusiana na kuyaelewa mashati ya ndoa ya muda mfupi, namba ya swali katika tovuti ni 7664.