iwapo mtu atawajibikiwa kufunga mwezi wa Ramadhani, naye kwa makusudi akabakia na janaba hadi adhana ya asubuhi, anaweza yeye akatayamamu katika nyakati za mwisho kabisa kabla ya kuadhiniwa adhana hiyo badala ya kuoga, kwa kuwa wakati wa kuoga haupo tena, kisha aendelee na funga yake, na funga hiyo itakuwa ni sahihi, ingawaje yeye atakuwa amefanya kosa kwa kule kubakia na janaba hadi wakati huo bila ya kuoga. Ama iwapo yeye atakuwa hakuoga, na akawa amefanya hivyo kwa makusudi, na kutayamamu pia akawa hakutayamamu, hapo funga yake itabatilika (itaharibika), na atawajibika kuifunga funga hiyo kwa kuilipa na pia atatakiwa kutoa fidia.[1]
[1] Taudhihul- Masail, kilichoshereheshwa na Imam Khomeiniy, juz/1, uk/908, suala la 1619, lisemalo: iwapo kwa makusudi mtu atabakia na janaba hadi adhana ya asubuhi bila ya kukoga, apia iwapo wadhifa wake ukawa ni kutayamamu lakini pia akawa hakutayamamu, huyo atabatilikiwa na funga yake. Pia rejea kitabu Ajwibal- Istiftaat, juz/1, uk/133.