Please Wait
8524
1- safari itakayo fanywa baada ya adhuhuri huwa haiharibu funga, na funga ya siku hiyo itakuwa sahihi.[1]
2- na mtu ambaye yuko safarini kisha akaamua kurudi kwake kabla ya adhuhuri, au akaamua kwenda sehemu ambayo ana nia ya kuweka makazi yake hapo kwa muda wa siku kumi, na pia akawa amefika sehemu aliyoikusudia kabla ya kuingia adhuhuri, huku mtu huyo akawa hakutenda tendo linalobatilisha funga, mtu huyo atatakiwa kuifunga siku hiyo, na funga yake ni sahihi.[2]
Kwa mfano: iwapo mtu ataondoka baada ya adhuhuri ya siku ya Jumamosi na kuelekea sehemu fulani, funga yake ya Jumamosi itakuwa ni sahihi,lakini iwapo yeye atataka kuifanya funga yake ya Jumapili pia kuwa ni sahihi, itambidi kurudi kwake au kuelekea sehemu ambayo anakusudia kuweka makazi ya yake kwa muda wa siku kumi kabla ya kuingia adhuhuri na atatakiwa kufika hapo kabla ya adhuhuri. Na funga yake itakuwa ni sahihi iwapo yeye atakuwa hakutenda tendo la kuibatilisha funga hiyo, na anatakiwa kutia nia ya kufunga baada ya kuwasili kwake, hapo funga yake itakuwa ni sahihi.
[1] Sherehe ya imam Khomeiniy Taudhihul-masaaili, juz/1, uk/953, suala la 1721.
[2] Sherehe ya imam Khomeiniy Taudhihul-masaaili, juz/1, uk/954, suala la 1722, na uk/953, suala la 1721.