Please Wait
25133
- Shiriki
Tukilitazama suala la kufunga njiwa kibinafsi, tutalikutia kuwa suala hili halina matatizo na ni halali. Lakini pale sisi tutapolimbatanisha suala hili na haki za majirani au wanajamii, hapo tunaweza kulipa picha ya uhalali au uharamu kwa jinsi hali za jamii mbali mbali zinavyolitazama suala hilo. Baadhi ya wafugaji njiwa huwa wanasabisha aina mbali mbali za maudhi kwa majirani na wanajamii wenzao, hii ni kwa kutokana na aina maalumu za maudhi yanayoweza kupatikana kutokana na njiwa hao, katika hali kama hiyo basi sheria haitompa yeye ruhusa ya kufuga njiwa ndani ya jamii bila ya ridhaa za majirani zake.
Kwa kuzingatia madhara au maudhi mbali mbali tuliyoyaashiria hapo juu, wanazuoni mbali mbali wa Kiislamu wametoa jawabu zifuatazo:
Jawabu kutoka ofisi ya kujibu maswali ya kifiqhi ya Ayatu-Llahi Khamenei (Mungu Amhifadi):
Iwapo ufugaji wa njiwa huo utasababisha maudhi kwa wanajamii, au ukasababisha madhara na utendekaji wa madhambi fulani ndani ya jamii au kwa majirani (kama vile kuparamia kuta za watu kwa ajili ya kuwafuata watoto wa njiwa, n.k), au sheria za nchi zikawa haziruhusu kufanya hivyo, katika hali kama hiyo, suala hili litakuwa halifai.
Jawabu kutoka ofisi ya kujibu maswali ya kifiqhi ya Ayatu-Llahi Makaarim Shirazi (Mungu Amhifadhi):
Kwa kutokana na kuwa suala hili mara nyingi huwa ni lenye kuwaudhi majirani, au kwa mara nyengine huwa linasababisha kutendeka matendo ya haramu, kama vile kuchungulia ndani ya nyumba za watu, hivyo basi watu wanatakiwa kujitenga na suala hili la ufugaji njiwa kiholela.
Jawabu kutoka ofisi ya kujibu maswali ya kifiqhi ya Ayatu-Llahi Safi Gulpeigani (Mungu Amhifadhi):
Hakuna tazizo mtu kufuga njiwa na akacheza nao au kuwaangilia vile wao wanavyopaa angani, lakini iwapo kufuga njiwa huko kutapelekea mtu kupoteza wakati wake na kujishughulisha na njiwa hao kupita budi, au pia kusababisha kutendeka mambo ya haramu, katika hali kama hiyo suala hilo la kufuga njiwa litakuwa halifai.
Jawabu kutoka ofisi ya kujibu maswali ya kifiqhi ya Ayatu-Llahi Sistani (Mungu Amhifadhi):
Suala la kufuga njiwa bila ya kulichanganya na mambo mengine, huwa lifaa na halina tatizo.
Jawabu kutoka ofisi ya kujibu maswali ya kifiqhi ya Ayatu-Llahi Mahdi Hadawi Tehraniy (Mungu Amhifadhi):
Iwapo kufuga njiwa huko kutakuwa na malengo ya kuwatumia njiwa hao katika kutuma barura au ujumbe, au kuzalisha njiwa hao kwa ajili ya matumizi fulani yenye kukubalika kisheria, suala hili halitakuwa na matatizo na litafaa. Lakini iwapo mtu atafuga njiwa hao bila ya kuzingatia manufaa yanayokubalika kiakili, tendo hilo la kufuga njiwa hao halitofaa na ni makruhu (ni jambo la karaha kisheria) kufanya hivyo. Na iwapo tendo hilo la kufuga njiwa litawasababishia maudhi majirani zako, au kusababisha kutendeka matendo ya haramu, hapo basi wewe hutaruhusiwa kufuga njiwa hao.
Mwisho wa jawabu kuhusiana na swali hili.
Link na kiungo kitachokupeleka kwenye uwanja wa maswali na majibu ya kifiqhi, ni kiungo chenye kodi (1115).