Please Wait
13074
Iwapo sisi tutailelekea Qur-ani Tukufu, kisha tukaiuliza Qur-ani swali lifualato: je sisi tumeumbwa kwa ajili gani? Hapa tutaiona Qur-ani ikitujibu kwa kauli ifuatayo:
" وَ ما خَلَقْتُ الْجِنَّ وَ الْإِنْسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ. " Maana yake ni kwamba: (Mimi (Mola) sikumuumba mwanaadamu wa jini, ila tu kwa ajili ya kuniabudu mimi).
Nini maana ya ibada? Ibada maana yake: ni kule mtu kuwa mtumwa wa Mola. Kwa hiyo zile kazi zetu na mambo yetu tunayo yahesabu kuwa ni mambo ya kawaida, hayo yanaweza kutundumaa kwenye mkusanyiko na mfungo mmoja wa ibada.
Maisha ya ki-Mungu au kiucha-Mungu, ni kule mtu kuishi huku yeye akitenda matendo yake ya kawaida yanayo fungamana na maisha yake ya kila siku, kupitia nia yenye malengo ya kumridhisha Mola wake katika utendaji wake, pamoja na yeye kutenda matendo hayo chini ya misngi maalumu iyendayo sawa na matakwa ya Mola wake.
Iwapo sisi tutarudi kwenye Qur-ani, kisha tukaiuliza Qur-ani swali hilo ulilo liuliza, tutaiona Qur-ani hiyo ikitupa jawabu ifuatafo: " وَ ما خَلَقْتُ الْجِنَّ وَ الْإِنْسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ ". Maana yake ni kwamba: (Mimi (Mola) sikumuumba jini wala mwanaadamu, isipokuwa kwa ajili ya kuniabudu Mimi tu).[1] Nini basi maana hasa ya neno ibada? Wengi miongoni mwetu huwa tunalitumia neno ibada huku sisi tukifikia upenuni tu mwa maana hasa ya neno hili bila ya kuingia ndani ya maana halisi ya neno hilo. Watu wanapolisikia neno ibada, huwa wanadhania kuwa: maana ya neno hili ni ile maana tu yenye kulenga baadhi ya matendo fulani, kama vile: sala, funga, Hija na mengineyo.
Sisi hatuna ubishani katika kukubaliana na matendo hayo kuwa ni miongoni mwa ibada, lakini hivi mwanaadamu ameumbwa ili aje kutenda matendo hayo tu? Iwapo mtu atayaangalia malengo ya kuumbwa kwa binaadamu na kuyafungamanisha na matendo hayo tu tuliyo yataja hapo! Mtu huyo atayaona maisha ya mwanaadamu kuwa yamewekwa kwenye jela yenye mabano ya dhiki mno. Lakini iwapo sisi tutalipekua kwa makini neno ibada, tutalikuta neno hilo kuwa na maana zaidi ya vile sisi tulivyo lifikiria neno hilo, kwani maana halisi ya neno hilo ni: kule mtu kuwa katika utumwa wa Mola wake maishani mwake mwote. Sadrul-Muta-a-Llihiin ametoa ufafanuzi mzuri kuhusiana na ibada, yeye alisema kuwa: kiwango cha ibada ya kila mmoja wetu huwa kina kwenda sawa na kile kiwango cha elimu ya kila mmoja wetu juu ya kumtambua Mola wake. Yaani kiwango cha ibada na fungamano lililopo baina ya mja na Mola wake, huwa ni lenye kuenda sambamba na kile kiwango cha elimu alichokuwa nacho mja huyo. Kwa hiyo kila pale mja anapo komaa kielimu katika kumuelewa Mola wake, ndipo ibada ya mtu huyo inapokuwa na usafi wa hali ya juu zaidi. Na hali hiyo huwa inaendelea hadi kufikia kiwango cha yeye kuhitajiwa na Usilamu. Uislamu umetutaka sisi tufanye nini? Je hivi Uislamu umetutaka sisi kuishi maisha duni yenye aina mbali mbali za mabano ya madhila?! Hivi Uislamu unakutaka wewe usali masaa ishirini na nne? Kufunga kila siku! Kuomba dua tu! Jee Uislamu unatutaka sisi kushikamana na hayo tu, bila ya kujishughulisha na mambo mengine? Bila shaka hivyo sivyo mambo yalivyo. Jee Mitume na Mawalii wa Mungu (a.s) waliishi maisha kama hayo? Jee kuna mtu anaye dai kuwa Ali bin Abi Talib alikuwa akiomba na kuabudu usiku na mchana mfululizo?! Sio hivyo, ali bin Abi Talib alikuwa ni mwana siasa, jemedari wa kivita, mwanachuoni na mfanya kazi, yeye alikuwa akijituma kisawa sawa, na hata kazi ya kuchimba kisima pia alikuwa akiifanya, yeye alikuwa akichimba misingi ya maji kwa ajili ya kazi za kilimo na kuyafikisha maji hayo katika sehemu zinazo hitajika maji hayo kufika, yeye hakuwa akivuta uradi tu. Iko wapi basi ile ibada ya Ali tunayo msikia yeye kusifiwa nayo kila wakati? Hivi yeye alikuwa akiabudu pale alipokuwa akiomba dua tu? Kwani iwapo yeye atakuwa na kiasi kama hicho cha mishughuliko, basi yeye hatokuwa na wakati wa kumuabudu Mola wake!! Hapana sio hivyo! Bali Ali (a.s), alimuabudu Mola wake katika hali zote za matendo na amali zake za kila siku, shughuli zote zilizo fungamana na maisha yake zilikuwa ni ibada, hata pale yeye alipokuwa yumo vitani, alikuwa akimuabudu Mola wake, kama linavyo onekana hilo kwenye Hadithi isemayo:
" لضربة علیّ یوم الخندق افضل من عبادة الثقلین ". Maana yake ni kwamba: (Kile kipigo cha Ali kwenye vita vya Khandaq, ni bora na chenye uzito na usafi wa nia, kuliko ibada za watu na majini wote kwa ujumla.)[2] Usemi na lugha iliyo tumika katika Riwaya hii, haina nia ya kumpa kichwa au kumsifu tu Ali (a.s), bali huo ni ukweli usio pingika, na hilo linatokana na yeye mwenyewe kuwa ndio picha na kigezo kamili cha ibada, kwani maisha yake yote yalikuwa ni ibada. Hivyo basi sisi hapa, tutakuwa tumesha ifahamu maana halisi ya neno ibada, na lile swali lililo ulizwa kuhusiana na maana hasa ya maisha ya kiucha-Mungu, litakuwa tayari limesha jibika, na jawabu hasa ya swali hili ni kwamba: maisha ya kiucha-Mungu, ni kule mtu kuyatenda matendo yote yaliomo maishani mwake kwa nia ya kutafuta radhi za Mola wake, huku yeye akijitahidi ipaswavyo kuyatenda matendo yake kupitia ule mfumo ambao ni wenye kuendana sawa na mtakwa ya Mola Mtakatifu. Hayo basi ndiyo maisha ya kiucha-Mungu.
Pengine bado kutakuwa na swali kuhusiana na ule mtindo wa kuyatenda matendo kupitia mfumo uendao sawa na matakwa ya Mola. Usemi wetu huu unakusudia kuwa: mtu anapotaka kuishi maisha ya kiucha-Mungu, ni lazima atahadhari na kujitendea mambo kiholela, kwa mfano pale yeye anapotaka kula, ni lazima auangalie uhalali wa kile anachotaka kukila, kwani sio kila kitu ni chenye kufaa kuliwa. Mtu anaweza kukiona kitu fulani kuwa ni miongoni mwa vyakula vinavyoliwa, lakini ukweli ni kwamba sio kila chakula ambacho kiko katika jamii ya vyakula huwa chafaa kuliwa! Wewe hutakiwi kula mali ya haramu, chakula cha haramu (cha wizi) au kile kilichoharamishwa kwa sababu maalumu. Wewe unatakiwa kufanya juhudi za kutengana na hayo, pia pale ulapo chakula, unatakiwa kukila chakula hicho kwa nia ya kutafuta nguvu za kufanya kazi, kazi ambayo itakuwa na nia ya kuyatatua matatizo ya viumbe wenzako, unatakiwa kuzitumia nguvu na maarifa yako kwa kuwasaidia jamaa zako, mkeo pamoja na wanaadamu wengine ili waweze kuyaelekea matakwa ya Muumba wetu, wewe unataikiwa kufanya kazi ili uweze kuutekeleza wadhifa ulio nao, na hilo ndilo litakalo kifanya kitendo chako cha kula kuwa ni ibada. Iwapo maisha yetu tutayaweka katika picha hii ya mfumo wa Mola, hapo ndipo maisha yetu yatakapo geuka na kuwa ni maisha yenye nuru ya usafi wa roho.
Katika kutafuta jawabu muwafaka juu ya swali lako na ili tukupatia jawabo nono, sisi tumekuchagulia Riwaya maalumu ifuatayo ambayo imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w). Insemekana kuwa: siku moja Mtume (s.a.w.w) aliwaambia wafuasi wake: (Yule mwenye hamu ya kumuona mtu wa Peponi, basi amuangalie yule atakaye ingia mwanzo msikitini katika siku ya leo, pale alipokuwa akiyasema maneno hayo, alikuwepo kijana mmoja aliyekuwa na hamu sana ya udadisi juu ya yale maneno ya Mtume (s.a.w.w), yeye aliamua kusubiri ili amuone huyo mtu wa Peponi, muda si mrefu akatokea mtu mwenye umri wa uzeeni na kuingia ndani ya msikiti, yeye alimuangalia sana yule mtu, mwishowe akaaamua kutumia ujanja ili aweze kujua ni amali gani anayo ifanya mtu yule, hapo aliamua kumfuata na kubisha hodi, alipokarishwa alisema kuwa: mimi ni mgeni mpita njia, hapo yeye akakaribiswa kupumzika na yule mzee, yeye kila alipo muangalia yule mzee, hakumuona akitenda tendo maalumu, hapo alishangaa, akasema bila sha mtu huyu atakuwa anafanya ibada zake katika usiku wa manane, kwa hiyo yeye aliamua kukesha ili ayaone matendo ya mja huyu, lakini yule mzee alilala fofofo! Hadi wakati wa sala ya asubuhi ulipofika ndipo alipoamka na kusali sala ya asubuhi. Kijana yule alishangazwa sana, na mwishowe akashindwa kustahamili, hapo aliamua kumuelezea yale aliyo yasikia kutoka kwa Mtume (s.a.w.w), yule mzee akamjibu: kwa kweli mimi sijijui kuwa ni mto wa Peponi au vipi! Na wala sina amali yoyote ile maalumu ninayo ifanya, ila tu mimi pale nitendapo matendo yangu ya kila siku, huwa najitahi kuyatenda kwa nia safi ya kutaka radhi za Mola wangu, na pale ninapotaka kutenda jambo fulani, huwa ninajitahidi kuto muudhi Mola wangu ndani ya tendo hilo, ni hayo tu ndiyo niliyo shikamana nayo mimi, na wala sina jengine.)
Ni kweli kabisa ni hilo tu ndilo lilimfanya Mtume (s.a.w.w) kuwaambia Wafuasi wake kuwa yeye ni mtu wa Peponi. Hayo ndiyo maisha ya kiucha-Mungu, mtu anatakiwa asifanye jambo bila ya kutaka radhi za Mungu kupitia tendo hilo, sisi tusihangaike sana huku na kule kutafuta njia ya Peponi, njia ya Peponi imo humu humu ndani ya kazi zetu za maishani mwetu, tunachotakiwa kukifanya ni kutenda matendo yeto chini ya msingi wa matakwa ya Muumba wetu, na hapo ndipo rangi na harufu ya maisha yetu itapobadilika na kupendeza. Hilo ndilo liwezalo kuubadilisha mfumo wetu mzima wa maisha yetu. Bila ya sisi kuifanyia majaribio njia na mfumo huu tulio ufafanua hatutoweza kuuelewa ukweli na natija ya madai yetu. Mwana-Falsafa na Mfasiri maarufu wa Qur-ani ajulikanaye kwa jina la Tabaataai ansema: Hebu ifanyieni kazi ile Riwaya isemayo: "مَنْ أَخْلَصَ لِلَّهِ أَرْبَعِينَ يَوْماً فَجَّرَ اللَّهُ يَنَابِيعَ الْحِكْمَةِ مِنْ قَلْبِهِ عَلَى لِسَانِهِ" Maana yake ni kwamba: Mwenye kumsafia nia Mola wake katika matendo yake kwa muda wa siku 40, Mola atazichimbua chemu chemu za hekima kutoka moyoni mwake, kisha zitiririke kwenye ulimi wake.[3] Yeye aliendelea kusema: kwa kweli mimi nina yakini na Riwaya hii na nina iamini kiasi kikubwa mno, basi hebu na nyinyi ifanyieni kazi, na iwapo mtu ataifanyia kazi kisha akawa hakupata kile kilicho ahidiwa ndani ya Riwaya hii, basi aje kunilani. Mwisho wa kunukuu. Hebu basi na sisi tujifunge mkaja na tuamue kuifanyia kazi Riwaya hii. Tunamuomba Mola atuwafikishe katika kutenda yale yanayo endana na matakwa Yake. Aamin.
[1] Suratu Dhariaat, Aya ya 56.
[2] Iqbaalul-Aa’maal, cha Sayyid Ibnu Taawuus, uk/467, chapa ya Darul-Kutubil-Islaamiyya, Iran Tehran, mwaka 1367 Shamsia.
[3] Biharul-Anwaar, cha Muhammad Baaqir Majlisiy, juz/67, uk/249, chapa ya Al-Wafaa, Beirut Lebanon, mwaka 1404 Hijiria.