Please Wait
21757
Mtu anaweza kupatwa na janaba katika hali mbili: ima itakuwa ni kabla ya adhana ya asubuhi au baada ya adhana ya asubuhi, lakini janaba tunalolizungumzia hapo ni lile janaba la dharura, kama vile dharura ya kuota, siyo la kupiga ponyeto au kujamii.
Kukoga janaba kabla ya dhana ya asubuhi:
Kauli ya imam khomeiniy inasema: iwapo mtu atabakia na janaba kwa makusudi hadi wakati wa adhana ya asubuhi ukaingia, au iwapo yeye alikuwa anawajibika kutayamamu lakini akawa hakutayamamu, na akawa amefanya hivyo kwa makusudi, funga yake itabatilika.[1] Lakini iwapo yeye atakuwemo ndani ya funga nyengine ya wajibu maalumu, kama kama vile funga ya nadhiri, funga yake itakuwa ni sahihi.[2]
Kwa hiyo iwapo mtu atakutwa na janaba ndani ya saumu ya Ramadhani, na tokeo hilo likawa ni kabla ya adhana ya asubuhi, mtu huyo atatakiwa kukoga janaba.
Kukoga janaba baada ya adhana ya asubuhi na kuendelea kipindi kizima cha mchana:
Kauli ya imam Khomeiniy: iwapo mwenye funga ataingiwa na janaba ndani ya mchana (hali akiwa amelala), hakutokuwa na ulazima kukoga papo hapo[3], lakini atawajibika kukoga janaba pale atapotaka kusali adhuhuri, alasiri, magharibi au ishaa. Na wakati wowote ule mtu atakapoamka baada ya adhana ya asubuhi ndani ya mwezi wa Ramadhani, na akajikutia kuwa ana janaba, hata kama atakuwa anajuwa kuwa janaba hilo limempata kabla ya adhana hiyo, funga yake itakuwa ni sahihi.[4]
Kwa hiyo wakati wowote ule mtu akiwemo ndani ya saumu anaweza kukoga janaba.
[1] Taudhihul-masaail chenye sherehe ya imam Khomeiniy, juz/1, uk/908-909, suala la 1619. Kauli ya Makaarim Shirazi ni kwamba: ni wajibu kuchukuwa tahadhari ya kuihesabu funga yake kuwa ni batili, lakini iwapo atakuwa hana uwezo wa kukoga au akawa na dhiki ya wakati, anatakiwa kutayamamu, lakini iwapo atakuwa yeye hakufanya hivyo kwa makusudi, basi funga yake itakuwa ni sahihi. Kauli ya Faadhil Lankaraniy: mtu anayetaka kufunga Ramadhani au kulipa funga za Ramadhani, hatakiwi kubakia na janaba kwa makusudi hadi wakati wa adhana ya asubuhi, hivyo basi iwapo yeye atakuwa hakukoga na pia kwa kutokana na dhiki ya wakati akawa hakutamamu, funga yake itabatilika. Kukaa na janaba katika funga nyengine, iwe ni kwa makusudi au si kwa makusudi, huwa hakuleti madhara juu ya funga hizo. Kauli ya Safi Gulpeigaaniy: iwapo mtu atabakia na janaba ndani ya Ramadhani hadi adhana ya asubuhi bila ya kukoga, pia akawa hakutayamamu, lakini akawa hakuwa na makusudio ya kufanya hivyo, bali labda kulikuwa kuna mtu aliyemzuia kufanya hivyo, funga yake itakuwa ni sahihi.
[2] Rejea kitabu kilichopita, uk/909, suala la 1620. Kauli ya Khui na Tabriziy: iwapo yeye atakuwemo ndani ya saumu isiyokuwa ya Ramadhani au katika kuilipa funga ya Ramadhani, bali akawa katika saumu nyengine yenye kumuwajibikia yeye katika siku maalumu, kama vile funga ya nadhiri, funga yake inaonekana kuwa ni sahihi.
[3] Rejea kitabu kilichopita, uk/915, suala la 1632. Kauli ya Faadhil Lnkaraniy: ingawaje inapendekezwa mtu kuchukuwa tahadhari ya kukoga papo hapo. Kauli ya Makarim Shirazi: ni vizuri wakati wowote ule mwenye saumu anapopatwa na janaba kukoga papo hapo, lakini iwapo yeye atakuwa hakukoga papo kwa hapo, funga yake haitobatilika.
[4] Rejea kitabu kilichopita, suala la1633. Kauli ya Makarim Shirazi: funga yake ni sahihi, iwe anajuwa kuwa amepatwa na janaba kabla au baada ya adhana, au awe na shaka juu ya hilo.