advanced Search
KAGUA
51750
Tarehe ya kuingizwa: 2012/05/21
Summary Maswali
nini maana ya neno (dini)? Au dini hasa ni kitu gani?
SWALI
nini maana ya neno (dini)? Au dini hasa ni kitu gani?
MUKHTASARI WA JAWABU

Wamagharibi wametumia ibara mbali mbali ili kupata maana muwafaka inayowafikiana na neno (dini), na neno (dini) ndani ya Qur-ani limetumika huku likibeba maana mbili tofauti, nazo ni kama ifuatavyo:

1- dini ni aina yeyote ile ya itikadi yenye kulenga nguvu maalumu za ghaibu zinazoaminiwa na kundi fulani la waumini wa nguvu hizo, bila ya kugusia ubatili na wa imani hizo, kama ilivyokuja katika Qur-an:

« لكم دينكم ولى دين».

2- dini ni imani maalumu ya kumuamini na kumtii Mungu wa haki, kama ilivyoelezewa ndani ya Qur-ani pale iliposemwa:

«ان الدين عندالله الاسلام».

Katika makala hii tunapozungumzia maana ya neno (dini), huwa tunailenga maana hii ya pili ya neno hili, maana ambayo ni yenye kulenga tu ile itikadi ya kumuamini Mungu wa haki na kumtii, huku dini ikiwa na daraja mbali mbali, kama vile: dini iliyotufikia sisi na ile dini halisi ambayo bado sisi tupo katika njia ya kuifanyia utafiti wa ukweli wake na uhakika wake.

JAWABU KWA UFAFANUZI

Wamagharibi wamejaribu kutumia ibara tofauti ili kuifikia maana muwafaka na yenye kwenda sawa na neno (dini), John Hick ndani ya kitabu chake kijulikanacho kwa jini la (Falsafa ya dini), ameitaarifisha dini kwa kupitia mitazamo mbali mbali yenye kuegemea katika fani tofauti za elimu, na maana ya neno dini pamoja na ufafanuzi wake katika kitabu hicho ni kama ifuatavyo:

A- maana ya dini katika fani ya Saikolojia:”dini ni hali na hisia maalumu anayoipata mtu fulani pale anapokuwa yu peke yake, hali ambayo huwa ni yenye kuthaminiwa na kuaminiwa na mtu huyo kuwa inatokana na Mungu”. imenukuliwa kutoka kwa William James.

B- maana ya dini kwa mtazamo wa fani ya Elimu ya jamii: “dini ni idadi maalumu ya itikadi, matendo, alama pamoja  vitengo vya kidini ambavyo vimejengwa na wanajamii ndani ya jamii mbali mbali”. Imenukuliwa kutoka kwa Talcott Parsons.

C- maana ya dini kwa mtazamo wa Kipagani (Naturalism): “dini ni mlolongo wa amri na makatazo ambayo huwa ni vizuizi vinavyomfanya mtu kutokuwa na uhuru, vizuizi ambavyo huulemaza uwezo wetu wa kimaumbile”. Imenukuliwa kutoka kwa (Saloman Reinach).

Na Matthew Arnold naye naongezea kwa kusema:”dini ni ile tabia na hisia maalumu inayomfanya mtu kuhisi kuwa, kuna aina maalumu ya nguvu tukufu juu yake zinazomtawala, na hisia hizo walizonazo baadhi ya watu, ndizo zilizolikuza suala zima la kuwepo kwa dini”.

D- moja miongoni mwa maana za dini: “ni kukubali na kuamini kuwa: viumbe vyote vinatokana na Mungu, navyo ni madhihiriko ya nguvu za Mungu huyo, Mungu ambaye hawezi kudirikiwa na akili zetu kielimu.[1] Imenukuliwa kutoka kwa Herbert Hpencer.

Maana mbali mbali zilizonukuliwa kutoka kwa wataalamu mbali mbali wa Kimagharibi, ni sababu tosha iliyowafanya wataalamu wa Kimagharibi kukubali kuwa neno (dini) haliwezi kupata maana moja muwafaka yenye kukubaliwa na watu wote bila ya pingamizi, bali neno (dini) ni lenye kukusanya aina mbali mbali za itikadi tofauti ambazo kwa namna moja au nyengine huwa na aina fulani ya uhusiano baina yake. Na Ludwig Josef Johann Wittgenstein anaufananisha uhusiano huo kwa kusema: “uhusianao uliopo baina ya itikadi mbali mbali ni kama vile uhusiano wa kifamilia ulivyo[2].[3]

Qur-ani nayo imelifasiri neno (dini) katika maana mbili zifuatazo:

1- Aina yeyote ile ya itikadi juu ya nguvu maalumu za ghaibu iwe itikadi hiyo ni sahihi au si sahihi. Kama asemavyo Mola:

لكم دينكم ولى دين»[4]

2- Itikadi ya kumuamini na kumtii Mungu wa haki tu. Kama asemavyo Mola:

ان الدين عندالله الاسلام»[5]

Na sisi Waislamu tunapoyazungumzia masuala ya dini au kulizungumzia suala la dini yetu, huwa tunaikusudia maana ya pili ya neno hilo, maana ambayo huwa ni yenye kuilenga tu ile itikadi ya kumuamini Mola mmoja wa haki, na dini yaweza kufanyiwa utafiti katika nyanja tofauiti, kama vile utafiti wa dini ilioko mkononi mwetu kama vile ilivyotufikia mimi na wewe mkono kwa mkono, na ile dini asili kabla ya kutawanywa kwa kupitia mikono ya watu mbali mbali (dini halisi).

Kwa utafiti zaidi waweza kusoma kitabu:

Wilayat wa diyaanat chapa ya pili, cha Ayatullahi Mahdi Hadawiy Tehraniy, kilichochapishwa na kitengo cha uchapishaji cha Muasese Farhangiy Khaneye Khirad, Qum 1380 Shamsia

 


[1] Rejea tarjama ya Kifarsi ya kitabu (Falsafa ya dini) cha John Hick ya Bahram Rad, uk/22 hadi 23, iliyosahihishwa na Bahaud-Diin Khoramshahiy, iliyochapishawa na Intishaaraat Bainal-Milali Al-Huda, Tehran, 1372 Shamsia.

[2] Family Resemblance.

[3] Rejea kitabu (Falsafa ya dini) cha  John Hick, uk/22 hadi 23.

[4] Nyiyi mna dini yenu nami nina dini. Suratul Kaafiruun Aya ya 6.

[5] Hakika dini halisi mbele ya Mola, ni kusalimu amri (Uislamu). Suratu Aalu Iraan, Aya ya 19.

 

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

YALIYOSOMWA ZAIDI