Please Wait
19396
Neno (kupanga mipango ambalo kwa Kiarabu ni مکر), humaanisha utafutaji wa hila au njia katika kulifikia jambo fulani, na yawezekana mtu kutafuta hila na njia za kuyafikia mazuri au mabaya.
Ujanja wa Mungu: kuna Aya tofauti ambazo zimeliegemeza na kulinasibisha neno (ujanja مکر) kwa Mola Mtakatifu, na maana halisi ya neno hili ndani ya Aya hizo huwa inamaanisha maana ya upangaji wa mambo kiujumla jamala, kwani Yeye Ndiye Mmiliki wa njia zote za upangaji wa mambo, na wala hakuna njia yeyote ile ya upangaji wa mambo iliyoko nje ya uwezo na milki yake. Hivyo basi Mola ni mwenye daraja ya juu kabisa katika suala la upangaji kuliko aina zote zile za wapangaji wa mipango mbali mbali, na hilo limezungumzwa ndani ya Qur-ani pale Mola Aliposema: «اللَّه خير الماكرين», yaani Mola ni Mbora wa wapangaji, na katika Aya nyengine Mola Anasema: (Kabla yao vile vile kulikuwako wakorofi waliopanga mipango na njia mbali mbali (za uharibifu), lakini njia na mipango yote iko ndani ya uwezo wa Mola. Na Mola yanamuelea yote yale yatendayo na kila mja, na muda si mrefu makafiri watatambua kuwa hatima njema itamfikia nani!). Aya hii inatoa upeo wa wazi kabisa kuwa, mipango yote ipo kwenye uwezo Wake Mola, na mipango ya wapangaji wengine haiwezi kuwa na nafasi mbele Yake.
Neno (kupanga mipango ambalo kwa Kiarabu ni مکر), humaanisha utafutaji wa hila au njia katika kulifikia jambo fulani, na yawezekana mtu kutafuta hila na njia za kuyafikia mazuri au mabaya.[1]
Lakini neno hilo kwa wakati mwengine humaanisha kufanya ujanja na udanganyifu, vile vile neno hilo limenasibishwa na Mola huku likiwa na maana ya ujana na kuadhibu.[2]
"مكر الا لهى au ujanja wa Mola": tukiliangalia neno (مكر) namna lilivyokuja katika Aya tofauti za Qur-ani,[3] tutakutia kuwa neno hili limetumika ndani ya Qur-ani likiwa na maana ya upangaji wa mipango na utafutaji wa budi, lakini mara nyengi upangaji huo huwa ni kwa ajili ya kuleta madhara na wakati mwengine ukawa ni kwa ajili ya kuleta manufaa, kwa mfano katika Aya isemayo: «وَ يمكرون و يكمر اللَّه واللَّه خَير الماكِرين» yaani “wao ni wenye kupanga mipango kwa nia ya madhara, lakini Mola ni Mbora zaidi wa wapangaji wa mipango (iwe ya madhara au ya kuleta faida)”.[4] Maana ya wao kufanya ujanja kunamaanisha kule kupanga kwao mipango maalumu kwa ajili ya kumua Mtume (s.a.w.w) au kumuekea kwa vikwazo mbali mbali, na maana ya neno "يَمكُرُ اللَّهُ" humaanisha kule Mola kuwa ni mwenye kupanga mipango maalumu ambayo ilimuamuru Mtume (s.a.w.w) kuhamia Madina. Na kama utaiangaza Qur-ani kwa makini, utalikutia neno مكر)) ndani yake likipewa sifa ya ubaya kwa kuitwa السَّيِئّى) مکر) jambo ambalo litakufahamisha kuwa kuna aina mbili za upangaji wa mipango, nazo ni upangaji wa mipango kwa ajili ya wema au manufaa na upangaji wa mipango kwa ajili ya madhara fulani.[5] La kuzingatia hapa ni kwamba pale neno hili linapotumika ndani ya Qu-ani huku likinasibishwa na Mola, huwa lina maanisha kuwa Mola Ndiye Aliye Mmiliki wa aina zote zile za upangaji, na wala hakutatokea njia au mipango itakayoweza kukaa njie ya uwezo na milki Yake (s.w). Na hiyo ndiyo maana ya kuwa Yeye yuko juu zaidi kuliko wapangaji wote wengine waliopo au wanaokadiriwa kuwepo.[6] Aya ilioko katika Surat Raad[7] iko wazi kabisa katika kuufikisha ujumbe huo unao onyesha kuwa: Yeye ndiye aliye miliki aina zote zile za upangaji, na wapangaji wengine wote hawana uwezo wowote ule mbele ya upangaji Wake Yeye (s.w).[8]
[1] Qamusi ya Qur-ani ya Sayyid Ali Akbar Qurashiy/ juz: 6/ uk: 265.
[2] Almunjid kilichotarjumiwa na Muhamed Bandar Rikiy, juz: 2/ uk: 1820.
[3] Rejea Suratul Aaraaf Aya ya 99 na 123, Faatir 10 na 43, Raad 33 na 42, Sabaa 33, Yuunus 21, Aal-Imraan 54, Nahl 26 na 45, Naml 50 na 51, Nuuh 22, Ibrahim 46, Yusuf 13 na Ghafir 45.
[4] Anfaa,l 30.
[5] Faatir, 43.
[6] Aali-Imraan, 54.
[7] Raad, 42.
[8] Tafsiri Al-miizaan ya Sayyid Muhamed Husein iliyotarjumiwa na Musawiy Hamadani/ juz: 12/ uk: 355, chapa ya Intishaaraat Islami.