Please Wait
8916
watu kama hawa wanatakiwa kusali safari, na pia hawaruhusiwi kufunga katika hali kama hiyo, na wala hawawezi kufunga funga zao za nadhiri huku wakiwemo ndani ya mwezi wa Ramadhani tena safarini.
Lakini iwapo wao wataifikia sehemu walioikusudia kwenda kubaki hapo kabla ya kukengeuka kwa jua, basi siku hiyo watawajibikiwa wafunge, huku ikizingatiwa kuwa wao kabla ya kufika hapo pahala watakuwa hawakutenda tendo la kufunguza (kubatilisha saumu), katika hali kama hiyo, funga ya siku hiyo itakuwa ni sahihi.
Nyinyi funga zenu zitakuwa hazikubaliki katika hali kama hiyo, na pia mnatakiwa kusali safari, na baada ya Ramadhani mtakuja kuzilipa funga zenu, na hilo ni lenye kwenda sawa na hukumu zilizotolewa na maulamaa kama vile Imam Khomeiny (r.a), pale aliposema kwamba: wanaoweza kufunga huku wakiwa safarini, ni wale tu ambao kwao wao safari zimeshakuwa ndio kazi zao, kama vile marubani, madereva, na wachungaji ambao wao siku zote wako kiguu na njia kutoka sehemu moja kwenda nyengine wakitafuta malisho ya wanyama wao.[1] Kwa hiyo hukumu yenu nyinyi haifanani na watu wa aina hiyo, hivyo basi mnatakiwa kula na kusali safari, na baada ya Ramadhani mtakuja kuzilipa funga zenu. Na ili mtu ahesabiwe kuwa yeye safari ndiyo imeshakuwa kazi yake, anatakiwa awe ni mwenye kusafiri mfululizo kwa kiasi cha muda wa miezi mitatu akienda na kurudi.[2] Na kwa sababu nyinyi hamuko safarini zaidi ya mwezi mmoja, basi hamtakiwi kufunga.
Na kuhusiana na suala lenu lisemalo kuwa je mnaweza kunga saumu ya nadhiri huku mkiwa ndani ya hiyo safari yenu? Jawabu ni kwamba: kwa kutokana na fatwa za Imam Khomeiny, ni kuwa iwapo mtu atakuwa ameweka nadhiri ya kufunga safarini, basi anatakiwa kuitimiza nadhiri yake hiyo akiwemo safarini. Na iwapo atakuwa ameweka nadhiri ya kufunga siku maalumu akiwepo safari au nymbani, basi ifikapo siku hiyo itambidi afunge katika hali yeyote ile, iwe yupo safarini au yupo ndani ya mji wake.[3] Lakini amali za wajibu hazikubali kuwekewa nadhiri, kwa hiyo haiwezekani mtu kuweka nadhiri ya kufunga Ramadhani huku akiwa safarini, wala haikubaliki mtu kuweka nadhiri ya kufunga funga ya nadhiri fulani ndani ya Ramadhani.
Ama khusiana na wale watakaofika mjini kabla ya kukengeuka kwa jua, Imam (r.a) pamoja na maulamaa wengine wote wanasema kuwa:
Iwapo mtu ataingia mjini kwao kabla ya kukengeuka kwa jua, au akafika kwenye mji ambao ana nia ya kukaa ndani yake kwa muda wa siku kumi, huku akiwa mtu huyo bado amefika sehemu hiyo bila ya kufungua au kutenda tendo la kufunguza, funga yake itakuwa ni sahihi, na iwapo yeye atakuwa ametenda tendo la kufutarisha kabla ya kufika mahala hapo, huyo basi hatokuwa hana funga kwa siku hiyo, na anatakiwa kuja kuilipa funga ya siku hiyo baada ya Ramadhani.[4]
[1] Taudhihil- Masaail cha Imam Khomeiny, juz/1, uk/701. Ambapo amesema: sharti ya saba ya mtu kufungua, kuwepo safarini, huku akiwa yeye hahesabiki kuwa safari ndiyo kazi yake, kwa hiyo wachungaji, madereva, marubani na wanaofanana nao, hata kama watakuwa wamo safarini kwa ajili ya kuupeleka mzigo wao wenyewe, pia hawawezi kuruhusiwa kula au kusali safari, isipokuwa tu katika ile mara yao ya kwanza ya kuanza kazi hiyo ya udereva hapo wataruhusiwa kufungua na kusali safari.
[2] taudhihul- Masaail cha Imam Khomeiny (r.a), juz/1, uk/704, suala la 1310, lisemalo: mtu ambaye ndani ya mwaka atakuwa ni mwenye kusafiri mara kwa mara, na hata kama atakuwa ni mwenye kuikodisha gari katika kiezi kadhaa ya mwaka, mtu kama huyu anaposafiri kwa kutumia gari yake au isiyokuwa yake anatakiwa kufunga na kusali sala kamili bila ya kupunguza. Na pia ni vizuri kwake kusali aina zote mbili za sala, yaani sala ya msafiri na ya mtu wa kawaida kwa pamoja.
[3] Taudhihul-Masaail cha Imam Khomeiny (r.a), juz/1, uk/952, suala la1717.
[4] Taudhihul-Masaail cha Imam Khomeiny (r.a), juz/1, uk/954, suala la1722.