advanced Search
KAGUA
5173
Tarehe ya kuingizwa: 2018/11/05
Summary Maswali
Nini hukumu ya mwenye kumpa chakula muislamu asiyefunga?
SWALI
Nini hukumu ya mwenye kumpa chakula muislamu asiyefunga?
MUKHTASARI WA JAWABU
Si tatizo mtu kumpa chakula wakati wa mchana muislamu asiyefunga ndani ya mwezi wa Ramadhani. Hukumu hii na kwa yule muislamu amedharurika kufunga. Kama vile kumpa chakula wakati wa mchana muislamu aliye mgonjwa au msafiri. Kwa upande wa pili; ni vyema kutompa chakula muislamu asiyeruhusika kula (asiye kuwa na dharura zinazokubalika kisheria), ili mtoaji huyo wa chakula asije hisabika kuwa yeye ni mwenye kumsadia mtu huyo katika ovu hilo la kula mchana ndani ya mwezi wa Ramadhani. Ikiwezekana pia ni vyema mtu kumuwaidhi (kumnasihi) mtu huyo kwa lugha njema na mawaidha laini.
Nadharia za baadhi ya wanazuoni juu ya jambo hilo:
Mtazamo wa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei; Iwapo mja atawajibikiwa na funga, kisha akawa hakufunga bila ya kuwa na dharura yenye kukubalika kisheria, basi ni makosa mtu kumpa chakula mtu kama huyo.
Mtazamo wa Ayatullah Makarim Shirazi; Si tatizo mtu kumpa chakula aliyedharurika kufunga wakati wa mchana wa Ramadhani, iwapo mtu huyo atakuwa ameruhusika kisheria kuacha kufunga. Ni vyema kwa yule aliyewacha kufunga bila ya dharura za kisheria kunasihiwa na kuwaidhiwa kwa ulimi laini, na wala haitakiwi mtu huyo kumpa chakula wakati wa mchana.
Mtazamo wa Ayatullah Nuri Hamadani; Iwapo mtu huyo aliyewacha kufunga ni mwenye dharura, basi hapana tatizo kumpa chakula mtu huyo wakati wa mchana.
Mwisho wa jawabu, twategemea utaridhika na jawabu hii.
Ahsante sana.
TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

YALIYOSOMWA ZAIDI