advanced Search
KAGUA
8754
Tarehe ya kuingizwa: 2009/08/31
Summary Maswali
kuna ulazima gani wa kuonekana kwa mwezi kwa ajili ya Ramadhani? Na mbona suala hilo hailizingatiwi sana ndani ya miezi iliyobakia?
SWALI
kwa nini unapoingia mwezi wa Ramadhani huwa linasisitizwa sana suala la kuonekana kwa mwezi, huku suala hilo likiwa halionekani kupewa kipau mbele ndani ya miezi mingine? Je ndani ya miezi iliyobakia huwa kakuna ulazima wa kuzitekeleza ibada fulani, au kuadhimisha kwa makini matokeo fulani yaliyotokea ndaya ya baadhi ya miezi hiyo, kama vile matokeo ya mwezi wa Mharram?
MUKHTASARI WA JAWABU

Suala la kuonekana kwa mwezi ni lenye umuhimu ndani ya miezi yote, lakini suala hilo huwa ni lenye kupewa kipau mbele zaidi ndani ya mwezi wa Ramadhani, kwa kutokana na ulazima wa ibada ya funga iliyomo ndani yake, ambayo ni ya wajibu kwa Waislamu wote, pia suala hilo huwa na umuhimu kwa kutokana na uharamu wa kufunga saumu ndani ya siku ya Idi. Kwa hiyo si ndani ya mwezi wa Ramadhani tu watu huwa ni wenye kulizingatia jambo hilo, bali suala hilo hupewa kipau mbele pia katika mwezi wa Dhul- Hijja, kwa kutokana na ile ibada ya hija. Ndani ya miezi kama hiyo utawaona Waislamu wameshughulika sana katika kulifahamu suala la kuandama kwa mwezi, ili waweze kufahamu kuwa je tayari wameshawajibikiwa na ibada hiyo au la? Na  kinachooneka hapo ni ile hali ya mtu kujihisi kuwa na uzito fulani ulioko juu ya shingo yake ndani ya miezi fulani, miezi ambayo mja huwa anakabiliwa na aina maalumu ya ibada, hali ya kuwa suala hilo huwa halipo ndani ya miezi mingine, na wala mtu huwa hajihisi kuwa na uzito fulani juu ya shingo yake ndani ya miezi iliyobakia. Na hata ndani ya mwezi wa Muharram, mtu huwa hajihisi kuwa ni mwenye jukumu mbele ya Mola wake, kwa kule kuitanguliza au kuichelewesha siku hiyo, yaani iwapo mtu atataka kuliadhimisha jambo fulani ndani ya mwezi fulani, huwa yeye hajihisi kuwa ni mwenye jukumu la kuitambua kwa makini siku ya kuliadhimisha jambo hilo.

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

YALIYOSOMWA ZAIDI