Please Wait
7839
Waandishi mbali mbali wa walioandika na kulizungumzia tokeo la Karbala, hawakutoa ufafanuzi wa kutosha kuhusiana na farasi wa Imamu Husein (a.s), bali walichokielezea ni kuwa, farasi huyu alijipakaa damu ya Imamu Husein (a.s), kisha akaelekea kwenye mahema huku akitoa sauti kali yenye kuashiria huzuni na hasira. Watu wa nyumbani kwake ambao wakuwa wamo kwenye mahema, walipoisikia sauti ya yule farasi, walitoka nje ya mahema hayo, na walipomuona yule farasi yuko katika hali ile, walifahamu kuwa Imamu Husein (a.s) tayari ameshauwawa.[1] Lakini baadhi ya waandishi wa hivi sasa wameelezea khabari nyengine kuhusiana na hilo, na miongoni mwa vitabu vilivyo elezea khabari za nyongeza kuhusiana na hilo, ni (Naasikhut-Tawaariikh) kilichoelezea kuwa, farasi huyu alisimama nje ya mlango wa kungia katika mahema, kisha akawa anakitwanga kichwa chake na ardhi hadi akafariki, na baadhi ya waandishi wengine wamesema kuwa, farasi huyu baada ya kuuwawa kwa Imamu Husein (a.s), alielekea katika mto Furaat kisha akijtupa ndani ya mto huo.[2]
[1] Rejea kitabu Aamaal cha Sheikh Saduuq, uk/163.
[2] Rejea kitabu Naasikhut-Tawaariikh cha Mirza Muhammad Taqiy Sepehriy, juz/6, uk/2.