Please Wait
9115
- Shiriki
Mitazamo ya maulamaa ni yenye kutofautiana kuhusiana na suala hili. Moja kati ya mitazamo hiyo, ni ule mtazamo unaowafikiana na baadhi ya Riwaya pamoja na vitabu vya Tarehe, mtazamo huu ni kama ifuatavyo: mwili wa Imamu Husein (a.s), umezikwa na mwanawe mpenzi na muaminifu, naye ni Imamu Zeinul-Aabidiin (a.s), ambaye aliuzika mwili huo katika ardhi maarufu ya Karbala, Imamu Sajaad (Zeinul-Aaabidiin) (a.s) alikuwa anaitambua hukumu isemayo (imamu haoshwi ila na imamu na wala hakafiniwi ila na imamu kama yeye), usemi huu basi ulimlazimisha yeye kutumia miujiza na kutoka katika jela ya ibnu Ziaad, jela ambayo alikuwa amefungwa ndani yake, kisha akaelekea Karbala kwa ajili ya kuwatambuwa mashahidi waliouwawa huko pamoja na kuwazika ipaswavyo, hivyo basi yeye (a.s) ndiye aliyechukua jukumu la kuuzika mwili wa wa baba yake (Imamu Husein) (a.s).
Imamu Ridha (a.s) pale alipokuwa alipokuwa akijadiliana na mtoto wa Abu Hamza, Imamu Ridha alimuuliza: hebu niambie hivi Husein bin Ali (a.s) alikuwa ni imamu? Akamjibu: ndio, Imamu akamwambia: basi ni nani aliyechukua jukumu la kumzika? Akaamjibi: Ali bin Husein (a.s), Imamu akamuuliza: hivi huyo Ali bin Husein alikuwa wapi? Akamjibu: alikuwa Kuufa (moja kati ya miji ya Iraq) katika jela ya mwana wa Ziad, ama bila ya wao kuwa na habari Yeye (a.s) aliweza kuenda Karbala, kisha akatekeleza jukumu la kumzika baba yake ambaye ni Imamu Husein (a.s), halafu akarudi tena kifungoni. Imamu Ridha (a.s) akamwambia: yule aliyempa uwezo Ali bin Husein kufika Karbala kwa ajili ya kumzika baba yake, kisha akarudi tena jela, pia anaweza kunipa mimi uwezo wa kwenda Baghdadi kwa ajili ya kumzika baba yangu, hali nikiwa niko huru.[1]
Kwa kutokana na Hadhithi hii, tunaweza kusema kuwa Imamu Sajaad (a.s) ndiye aliyeuzika mwili wa baba yake (a.s).
[1] Maisha ya Zeinul-Aabidiin (a.s), cha Abdu –Razzaaq Muqaddam Muusawiy, kilichotarjumiwa kwa Kipashia na Habiib Ruuhaaniy, uk/578, pia kitabu (Tahliil az zindegi name Imam Sajjaad (a.s) ambacho ni tarjama iliyotoka katika Kiarabu kwenda Kipashia kupitia Muhammad Ridha Ataai, juz/1, uk/243.