Please Wait
14509
Tokeo hilo linaweza kutokea katika sura tatu, nasi tutazifafanua sura hizo na kuzijibu kwa mujibu mitazamo ya maulamaa isemavyo. Na jawabu zetu ni kama ifuatavyo:
1- iwapo mtu ataacha kufunga kwa kutokana na maradhi, kisha maradhi hayo yakaendelea hadi akafikiwa na Ramadhani ya mwaka wa pili, mtu huyo hatowajibikiwa kuzilipa funga hizo, bali atatakiwa kuzilipia fidia, na kiwango cha fidia hiyo kwa kila siku moja ni gramu 750 za ngano, mchele au kinachofanana na hivyo, na fidia hiyo inatakiwa kupewa mafakiri, lakini ni vizuri kutoa gramu 1500 kwa kila siku moja iliyompita.[1]
2- iwapo mtu atakuwa haweza kuzilipa funga hizo kwa udhuru mwengine, kama vile kuwa safarini, kisha udhuru huo akabaki nao hadi akaingiliwa na Ramadhani ya mwaka wa pili, huyo atatakiwa kuzilipa funga hizo na pia ni vizuri kuzilipa kwa kuzifunga na kuzilipia fidia, yote mawili kwa pamoja, na fidia hiyo ni kumpa fakiri gramu 750 za chakula kilichotajwa katika suala namba moja kwa kila siku moja.[2]
3- iwapo mtu ataacha kufunga kwa kutokana na udhuru fulani, kisha udhuru huo ukamuondokea baada ya kwisha Ramadhani, lakini yeye kwa makusudi akaacha kuzilipa funga hizo hadi kufikia Ramadhani nyengine, yeye atatakiwa kuzilipa funga hizo kwa kuzifunga, pia atatakiwa kuilipia kila siku moja kiwango cha gramu 750 za chakula na kumpa fakiri au mafakiri iwapo kiwango cha fidia hizo zitakuwa ni zaidi ya chakula cha fakiri mmoja.[3]
[1] Sherehe ya imam Khomeiniy Taudhihul-masaaili, juz/1, uk/947, suala la 1703.
[2] Sherehe ya imam Khomeiniy Taudhihul-masaaili, juz/1, uk/947, suala la 1703.
[3] Sherehe ya imam Khomeiniy Taudhihul-masaaili, juz/1, uk/947, suala la 1705.