advanced Search
KAGUA
12769
Tarehe ya kuingizwa: 2011/01/08
Summary Maswali
kuna njia gani za kujenga urafiki na Qur-ani zitakazo mfanya mtu azoeane na Qur-ani?
SWALI
kama kuna mtu atakaye omba nasaha kutoka kwenu zitakazo mfanya yeye avutiwe na Qur-ani na aipende, nyinyi mtampa nasaha gani?
MUKHTASARI WA JAWABU

Kama mtu atakaye isoma Qur-ani kwa nia ya kutafuta radhi za Mola wake, huku yeye akawa anaisoma Qur-ani hiyo kwa makini na kuitafakari vilivyo, basi Qur-ani iatamvuta mtu huyo na kumfanya awe ni mpezi wake wa rohoni.

JAWABU KWA UFAFANUZI

Qur-ani ni yenye athari kubwa kwa yule atakaye isoma ujanani, amipokewa Hadithi kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s) yenye kuonesha uongofu wa daima unao patikana katika kushikamana na Qur-ani tangu ujanani, na Hadithi hiyo ni kama ifuatavyo: (kijana yeyote yule mwenye imani atakaye dumu katika kusoma Qur-ani, Qur-ani itachanganyika naye na itapenya kwenye damu na nyama ya kijana huyo, naye atasimama katika safu za Malaika, na Qur-ani itakuwa ndio mlinzi wake wa siku ya Kiama… na yule atakaye taabika kwenye njia hiyo, basi ujira wake utapindukia na kupinfdukia zaidi.[1]

Likini pia tusisahau kwamba: yule atakaye pata faida za kiroho kutoka katika Qur-ani, ni yule atakaye isoma Qur-ani huku akiwa ni mcha Mungu, kwani ucha Mungu ndio sharti kuu la kuneemeka na Qur-ani. Sisi tuantakiwa kufungamana na Qur-ani, na fungamano hilo hukamilika kupitia mambo mawili, nayo ni kuisoma Qura-ani kwa tafakuri makini, na la pili ni kuyafanyia kazi mafunzo tunayo yapata kutoka katika Qur-ani hiyo, na hilo ndilo jambo msingi litakalo muezesha mtu kuzikwea daraja za juu zaidi zinazopatika katika Qur-ani, na bila ya wewe kushikamana na hayo, basi hakutokua na hata aina moja ya nasaha zitakazo kuwezesha wewe kukaa karibu na Qur-ani na kuneemeka nayo.

Ili tuelewane zaidi, mimi nakusihi uziangalie kwa makini Aya zifuatazo:

وَنُنَزِّلُ مِنَ الْقُرْآنِ مَا هُوَ شِفَاءٌ وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ ۙ وَلَا يَزِيدُ الظَّالِمِينَ إِلَّا خَسَارًا ﴿٨٢﴾

Maana yake ni kwamba: (Nasi tunashusha kutoka katika Qur-ani yale yenye tiba na rehema kwa waumini, lakini kwa wasio kuwa waumini, hilo haliwaongezei ila hasara tu.)[2]

قُلْ هُوَ لِلَّذِينَ آمَنُوا هُدًى وَشِفَاءٌ ۖ وَالَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ فِي آذَانِهِمْ وَقْرٌ وَهُوَ عَلَيْهِمْ عَمًى ۚ

Maana yake ni kwamba: ( Waambie (ewe Muhammad) kuwa: hii Qurani ni uongofu na tiba kwa waumini, na wale waiso amini masikio yao yana uziwi, na kwa hali yao walio kuwa nayo, Qur-ani itazidi kuwakandamiza katika upofu wao wa makusudi.)[3]

فَذَكِّرْ بِالْقُرْآنِ مَن يَخَافُ وَعِيدِ ﴿٤٥﴾

Maana yake ni kwamba: (…Basi itumie Qur-ani kwa ajili ya kuwakumbusha wale wenye kuikhofu adhabu (ya siku ya Kiama).)[4]

Aya zilizopita hapo juu, zote kwa pamoja ni zenye kutoa masisitizo ya kuwa: Qur-ani ni kitabu cha uongofu, lakini kitabu hichi ni chenye kuwatibu na kuwatakasa wale tu wenye malengo na nia safi ya kutaka kufahamu, na wala Qur-ani haina nia ya kuwatoza nguvu wasiotaka kuelewa. Ili basi mtu aweze kuifahamu Qur-ani kisawa sawa, ni lazima aisafishe nafsi yake na aiweke mbali na uwanja wa kishetani, ndiyo maana Mola akatuamrisha kujilinda na Shetani kabla ya kuanza kusoma Qur-ani.[5] Ili pia mtu aweze kupata uongofu kupitia Qu-ani, anatakiwa pale yeye anapozifikia zile Aya zenye kumpa yeye ukumbusho na maonyo, isiwe anaufumbia macho ukumbusho huo na maonyo hayo,[6] bali yeye anatakiwa ajute na alie kwa unyenyekevu wenye nia ya kutaka radhi za Mola wake, na asujudu mbele ya Mola huyo.[7] Na ni sifa za Waumini kuwa: pale wao wanapo zisikia Aya za Qur-ani, viungo vyao huwa vinatetemeka, miili na mioyo yao hulainika kwa kule kumkumbuka Mola wao, nao huwa tayari kwa ajili ya kuzipokea daraja za juu zaidi zitakazo wazidishia imani.[8]

Hayo ndiyo masharti ambayo mtu anatakiwa kuwa nayo, na hapo ndipo yeye atakapo weza kuifanya Qur-ani kuwa pamoja naye maishani mwake hadi siku ya Kiama. Na kama mtu ataisoma au atajifunza Qur-ani kwa malengo potofu, au kwa ajili ya kuifanyia shere na dhihaka, au pia kwa ajili kuyafikia malengo ya kidunia, mtu huyo hataweza kufaidika na Qur-ani hiyo na kupata ponyo la roho yake, bali yeye atakuwa na daraja ya chini kuliko hata yule asiye jifunza Qur-ani mbele ya Mola wake.

  Kuna Riwaya nyingi zinye kulitafiti fungamano linaloweza kupatika baina ya Wasomaji wa Qur-ani na Qur-ani yenyewe, na miongoni wa Riwaya hizo ni kama ifuatavyo:

  1. Mtume wa Mola (s a.w.w) amesema: (Wabora zaidi miongoni mwa wale wenye kufunga na kusali hadharani au kifichoni, ni wale walio ihifadhi Qur-ani vifuani mwao. Baada ya kusema hivyo alinyanyua sauti akasema: Enyi watu mlio ihifadhi Qur-ani vifuanai mwenu! Kuweni watiifu kupitia Qur-ani hiyo iliomo vifuani mwenu ili Mola wenu akuzidishieni neema zake, na wala msijifakhari kutokana na Qur-ani hiyo, ili Mola asije kukupigeni na chini, ifanyeni  Qur-ani kuwa ni pambo mbele ya Mola wenu ili Mola wenu akupambeni zaidi, na wala msiifanye Qur-ani kuwa ni pambo lenu mbele ya watu wengine, ili Mola wenu asije kukuporomosheni. Yule atakaye isoma na kuitumia vizuri Qur-ani, ni mfano kwamba: yeye ameumimina ujumbe wa Wahyi kifuani mwake bila ya yeye kufungamana moja kwa moja na chanzo cha Wahyi. Yule atakaye kuwa pamoja na Qur-ani, hatokuwa na tabia za kijahili pale yeye atakapo kutana na wale wasiokuwa na elimu, yeye hatokasirika kwa kutokana na hasira za watu juu yake, yeye huwa si mpapuraji pale anapokutana na wapapuraji au watu wanapogombana naye, bali yeye huonekana kuwa ni mwenye subira na usamehevu alio jifunza kutoka katika Qur-ani…)[9]
  2. Imamu Baaqir (a.s) amesema: kuna aina tatu za wasomaji wa Qur-ani:
  • Wale wenye kuisoma Qur-ani kwa ajili ya kujitafutia rizki, ambao huisoma Qur-ani mbele ya viongozi huku wakijionesha na kujifakharisha mbele ya watu wengine.
  • Wale wenye kuisoma Qur-ani huku wakizingatia hukumu Tajwidi kiswa sawa, lakini wakawa hawana aina yeyote ile ya mazingatio juu ya malengo yanayo kusudiwa ndani ya zile Aya wanazozisoma, hao hawatopata nyongeza yoyote ile kutoka kwa Mola wao!
  • Wale wenye kuisoma Qur-ani kwa ajili ya kutafuta ponyo la Qur-ani hiyo ili walitumie katika kuzipoza nyoyo zao, huku usiku na mchana wakijishughulisha nayo, wakawa ni wenye kuitumia kwa ajili ya kusimamisha sala zao za usiku na kutengana na vitanda vyao. Kundi hili la wasomaji ndilo lenye kupata baraka za Mola wao, Mungu huwaepusha na mabalaa na huwaweka mbali na maadui zao, pia mvua za rehema hunyesha kwa ajili yao.[10]
  • Jabir amenukuu ya kwamba: siku moja yeye alikuwa akizungumza na Imamu (a.s), kamawambia Imamu (a.s) ya kuwa: kuna baadhi ya watu pale wanaposoma au kuisikia Qur-ani ikisomwa, hujiangusha na kujifanya kama vile wametokwa na fahamu (kwa ajili ya kuwazuga watu), hadi watu wakaamini kuwa: hata kama wao watawakata moja kati ya viungo vyao! Basi hawatozindukana! Imamu (a.s) akajibu kwa kusema: Subhaan-Llah! Huu ni mtindo wa kishetani, na wala Mola hakuwataka wao wafanye hivyo. Kisomo kinatakiwa kiwe nyororo, chenye mbawa nyepesi (zitakazo muezesha mja kupaa kwenye anga za kimaana), na pia kiwe ni chenye kutoa machozi kwa kule kumkhofu Mola Subhaanahu Wataa’la.[11]

Naona tayari ufafanuzi huu umeshatosha katika kuwafahamisha watu hali halisi anayo takiwa kuwa nayo msomaji Qur-ani. Mola atuwafikishe tuw miongoni mwao. Aamin.


[1] Al-Kafi, cha Muhammad bin Yaa’quub Koleiniy, juz/2, uk/603, chapa ya Darul-Kutubil-Islaamiyya, Tehran, mwaka 1365 Shamsia.

[2] Aya ya 82, Suratul-Israa.

[3] Suratu Fussilat, Aya ya 44.

[4] Auratu Qaaf Aya ya 45.

[5] Suratun-Nahli, Aya ya 98.

[6] Suratul-Furqaan, Aya ya 73.

[7] Suratu Maryam, Aya ya 58, Israa, 107 hadi 109.

[8] Suratuz-Zumar, Aya ya 23.

[9] Usulil-Kafi, juz/2, uk/604, pia hayo unaweza kuyasoma kutoa katika juz/5 ya kitabu hicho.

[10] Rejea iliopita, uk/627, juz/1.

[11] Rejea iliyopita, juz/1, uk/616.

 

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

YALIYOSOMWA ZAIDI