Please Wait
14258
Ufafanuzi juu ya swali lako ni kwamba: jua ni moja kati ya vitu vyenye kutoharisha, na miongoni mwa vitu vyenye kutoharishwa na jua ni: ardhi pamoja na kuta za nyumba.[i]
Ili jua liweze kutoharisha ardhi na pamoja na zile kuta za nyumba zilizonajisika, ni lazima kuwe hakuna kizuizi juu ya ardhi au kuta hizo wala ndani ya kuta hizo, kwa mfano iwapo kuta au ardhi itakuwa imenajisika na najisi hiyo ikawa imepenya hadi ndani ya ardhi au kuta hiyo, basi iwapo kwa njia moja au nyengine, kukawa kumewekwa kuzuizi kitachoigawa ardhi au kuta hiyo katika tabaka mbili, na kizuizi hicho kikawa kati na kati ya tabaka mbili hizo za ardhi au kuta, katika hali kama hiyo kuta na ardhi hiyo itatoharika sehemu ya tabaka la juu tu, na tabaka la chini litabakia kuwa ni najisi. Pia ili jua liweze kutoharisha, basi hakutakiwi kuwepo kizuizi juu ya ukuta au ardhi kama vile pazia au bao fulani. Vile vile iwapo kwenye ardhi au kuta kutapatikana uwazi utakao igawa sehemu mbili kuta au adrhi hiyo, huku uwazi huo ukawa kati na kati baina ya sehemu mbili zilizo najisika, yaaani sehemu ya nje na ya ndani, basi uwazi huo utazuia juwa lisiweze kuitoharisha ile sehemu ya ndani ya kuta au ardhi hiyo iliyonajisika.[ii] Lakini pia wanazuoni wengine hawakuzitaja sharti kama hizi katika ufafanuzi wao juu ya hali ya jua katika kuvitoharisha vitu kama hivyo.[iii] Pia kuna wanazuoni wengine wanaoamini kuwa: jua haliwezi kuzitoharisha kuta za nyumba.[iv]
[i] Taudhihul-Masaaili cha sayyid Ruhu-Llahi Khomeiniy kilichohakikiwa na kusahihihshwa na Sayyid Muhammad Husein Bani Haashimiy Khomeniy, juz/1, uk/117, chapa ya nane ya Intishaaraat Islaamiy, mwaka 1424 Shamsia.
[ii] Rejea rejeo lililopita, uk/118.
[iii] Rejea rejeo lililopita, uk/117 hadi uk/118, chini ya suala namba 191.
[iv] Miongoni mwa wanazuoni hao ni Ayatu-Llahi Makaarim Shirazi, yeye anasema kuwa: juwa huwa linatoharisha ardhi pamoja na mapaa ya nyumba, lakini si jambo lenye yakini kuwa jua ni lenye kutoharisha kuta pamoja na milango ya nyumba au madirisha. Angalia kwenye kitabu kiitwacho: Taudhihul-Masaaili, kilichoshereheshwa na Imamu Khomeiniy, juz/1, uk/118.
Kwa ajili ya kupata ufafanuzi zaidi, rejea viungo na link zifuatazo kwenye tovuti yetu:
1- Swali la 4805: jua na utoharikaji wa nguo, mabrangeti na mazulia yaliyonajisika. Namba ya swali kwenye tovuti ni (5249).
2- Swali la 5002: sharti za kutoharika kwa kuta zilizonajisika kupitia jua. Namba ya swali ndani ya tovuti ni (5259).