advanced Search
KAGUA
4276
Tarehe ya kuingizwa: 2018/11/11
Summary Maswali
Kodi za yanayohusiana na maudhui
SWALI
Shati za kusihi kwa itikafu na sunna zake
MUKHTASARI WA JAWABU
 Kwanza tuwie radhi kawa kuchelewa kukujibu swali lako. Tuna tazizo wakati mwengine la kuchelewa kujibu maswali kwa haraka, hii ni kwa kutokana na kuzidiwa na maswali, au wafanya kazi wetu kuto kuwa na muda wa kutosha katika kujibu maswali mbali mbali.
JAWABU KWA UFAFANUZI
Itikafu ni ibada yenye masharti maalumu, masharti ya ibada hii ni kama ifuatavyo:
1- Imani ya Kiislamu
2- Kuwa na akili timamu
3- Kuweka nia ya ukuruba (kujipendekeza) kwa Mola Mtukufu. Hii ina maana ya kuwa; iwapo mtu atakaa itikafu kwa kujionesha mbele za watu, itikafu yake haitakuwa na thamani ya ibada, na wala hatopata thawabu za ibada hiyo.
4- Mwanzo wa kukaa itikafu ni kabla ya kuchomoza kwa alfajiri (kabla ya adhana ya sala ya asubuhi), na mwisho wa kikao cha itikafu kamili, ni hadi kuingia sala ya magharibi ya siku ya tatu. Ni lazima pia aianishe itikafu yake, yaani kama ni itikafu ya wajibu (kama itakuwa ni ya kuweka nadhiri), au ni itikafu ya mustahabbu (ya sunna), ni lazima kuiashiria kupitia nia iliyomo moyoni mwake.
5- Funga; kufunga ni wajibu kwa mwenye kukaa itikafu.
6- Uchache wa itikafu ni siku tatu; yaani itikafu yake isipunguge siku tatu, ama ikizidi zaidi ya siku tatu si tatizo. Itikafu isiyofikia kiwango cha siku tatu ni itikafu batili.
7- Itikafu iwe ndani ya msikiti mkuu unaozingatiwa na watu wa eneo alilopo; katika maeneo mbali mbali, mara nyingi huwa kuna misikiti midogo midogo tofauti, na huwa kuna misikiti maalumu ambayo huhesabiwa kuwa ni misikiti yenye kipau mbele zaidi. Itikafu yabidi ikaliwe kwenye misikiti mikubwa yenye kapau mbele zaidi.
8- Itikafu ni lazima idumu bila ya kukatishwa; yaani mwenye kukaa itikafu hataruhusiwa kutoka nje ya itikafu bila ya kuwepo dharura maalumu yenye kukubalika. Na hata kama atatoka kwa dharura, basi haitakiwi kukaa nje kwa muda mrefu, kiasi ya kwamba kiakili akawa amehisabika kuwa hayupo katika itikafu. Hii inamaanisha kwamba; iwapo atatoka nje na kubaki huko kwa muda mrefu kupita budi, itikafu yake itabatilika.
Sharti za itikafu
Yanayobatilisha itikafu ni kama ifuatavyo:
1- Yale yote yanayobatilisha funga ni yenye kubatilisha itikafu, kwani moja kati ya sharti za itikafu ni funga. Hii inamaanisha kwamba; iwapo funga itabatilika, pia itikafu nayo itabatilika.
2- Kutenda tendo la ndoa; iwapo mtu atatenda tendo la ndoa, itikafu yake itabatilika bila ya kuwepo tofauti baina kutenda tendo hilo wakati wa mchana au usiku.
3- Kupitia msingi wa kisheria wa kujitahadharisha na mambo yenye mashaka; ni wajibu mtu kujiepusha na yale yote ya haramu yanayobatilisha itikafu. Na iwapo atatenda moja kati ya matendo ya haramu yanayobatilisha itikafu, itikafu yake itabatilika. Lakini iwapo atatendo bila ya kukusudia bali kwa kusahau, itikafu yake itabaki salama (haitobatilika). Ila tendo la ndoa tu, tendo hili hubatilisha itikafu hata kama litatendeka bila kukusudia (kwa kusahau).
  Ni muhimu kutambua kuwa; iwapo mtu atabatilisha itikafu yake ya wajibu, kupitia moja kati ya mambo yanayobatilisha itikafu, itambidi ailipe itikafu hiyo. Pia kama ataibatilisha itikafu ya sunna ambayo imeshapitiwa na siku mbili za mwanzo, pia anawajibika kuilipa. Ama ikiwa ataibatilisha itikafu ya sunna kabla ya kumalizika siku mbili za mwanzo, yeye hatowajibika kuilipa itikafu hiyo.
Kafara za kubatilisha itikafu
Iwapo mtu ataibatilisha itikafu yake ya wajibu (ambapo yeye mwenyewe aliweka nadhiri kukaa itikafu hiyo). Kisha akaibatilisha kupitia tendo la ndoa. Mtu huyo ni lazima alipe kafara. Kafara ya itikafu ya wajibu ni sawa na kafara ya kufunja saumu ndani ya mwezi wa ramadhani. Na kama ataibatilisha itikafu hiyo kupitia tendo jenjgine lisilokuwa tendo la ndoa, pia atatakiwa kulipa kafara. Na kafara yake ni sawa na kafara ya kuvunja funga iliyo nje ya mwezi wa Ramadhani. Kafara ya kuvunja funga nje ya mwezi wa Ramadhani, ni kufunga siku tatu mfululizo.
Sunna za itikafu
Miongoni mwa Sunna za itikafu ni kama ifuatavyo:
1- Kukaa itikafu ndani ya mwezi wa Ramadhani, ni vyema pia kukaa ndani ya siku za kumi la mwisho la mwezi huo.
2- Kuchunga adabu na Sunna za Ramadhani katika itikafu.
3- Kujiepusha na dhambi za macho, masikio, ulimi pamoja na viungo vyengine.
4- Kujiepusha na choyo, husuda, kusengenya, tuhuma pamoja na mizozo.
5- Kuwa na huruma, subira, heshima, unyenyekevu, khofu mbele ya Mola wake, kujiepusha na waovu na kukaa mbali na washari.
6- Kuomba dua pamoja na kusoma Qur-ani.
Kutokana na watu wengi kukaa itkafu kwa pamoja, ni lazima basi mwenye kukaa itikafu kuchunga haki za kijamii ndani ya itikafu yake. Pia wakaaji itikafu ni lazima kuchunga haki za ibada na dua za pamoja. Ni jambo la lazima mtu kuheshimu watu waliolala msikitini humo, hivyo basi nyenendo zake zisije sababisha maudhi kwa wengine. Pia kuna mambo mawili muhimu yapaswayo kuzingatiwa;
A- Dua; Dua yenye kukubaliwa na Mola ni ile yenye unyenyekevu ndani yake, na ni vyema kuombwa kifichoni.
B- Kuheshimu na kuchunga haki za watu, ndio jambo la mwanzo kabla kutenda ibada zako. Kwa mfano mtu anaweza kua na hamu ya kusoma dua au Qur-ani kwa sauti kubwa, lakini jambo hili halikubaliki iwapo litasababisha maudhi kwa wengine.
Ni vyema basi mtu kusoma dua au Qur-ani kwa sauti ya chini, sauti ambayo haitasababisha maudhi kwa wengine.
 
TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

YALIYOSOMWA ZAIDI