Please Wait
10477
Ingawaje wengi miongoni mwa waandishi wa Historia hawakukinukuu kisa cha kuwepo kwa mtoto huyo wa kike wa Imamu Husein (a.s) mwenye umri wa kiasi cha miaka mitatu au mine, aliyejulikana kwa jina la Ruqayya au Fatimatu Sughra na baadhi ya wakati akijulikana kwa majina yasiokuwa hayo, lakini kuna vitabu maalumu vilivyo andikwa kuhusiana na maisha ya binti huyo vyenye kukinukuu kisa cha maisha yake yenye kusikitisha, pale yeye alipokuwa ndani ya mji wa Sham.
Pia katika vitabu vyetu vya Riwaya na Historia, kunapatikana maelezo kuhusiana na binti huyu, nasi tutazinukuu kauli mbili kutoka katika vitabu hivyo, ili kuitilia mkazo kauli yetu hii:
- Pale Zainab alipokabiliana na kichwa cha kaka yake (Imamu Husein) (a.s) huku yeye (Zainab) akiwa katika mji wa Kufa huko Iraq, alikisogelea kichwa hicho huku akisoma mashairi yenye maana ifuatayo: (Ewe ndugu yangu we! Hebu zungumza na huyu Fatima Sughra (Fatima mdogo), kwani moyo wake unakaribia kuvurugika…).
- Pale Imamu Husein (a.s) alipokuwa katika wakati wa mwisho wa maisha yake, ambapo alikuwa tayari ameshakabiliwa na upanga, alisema maneno yafuatayo: (Ewe Zainabu wangu! Ewe Sukaina wangu we! Ee wanangu nye! Ni nani atakayekusimamieni baada ya yangu mimi? Ewe Ruqayya wangu we! Ewe Ummu-Kulthumu wangu we! Nyinyi ni amana na dhamana kutoka kwa Mola wangu! Basi tambueni kuwa leo ahadi yangu imeshakaribia.
Sheikh Mufiid amesema kuwa: Sukaina alikuwa ni miongoni mwa mabinti wa Imamu Husein (a.s), na mama yake alikuwa akiitwa Rubaab.
Na Sheikh Tusi naye amenukuu kuwa: binti wa Imamu Husein (a.s) aliye julikana kwa jina la Sukaina, katika siku ya mapambano ya Ashura, yeye alikuwa na umri wa miaka kumi.
Na si hayo tu yalionukuliwa kuhusiana na binti huyo, bali kuna vitabu vyengine mbali mbali vilivyo zungumzia maisha yake.
Faida inayo patikana kutoka katika uhakiki tuliouona ndani ya Riwaya hizi ni kwamba: Imamu Husein (a.s) alikuwa na binti mwengine aliyejulikana kwa jina Sukaina, naye kabla ya kutokea tokeo la Ashura, alikuwa tayari amesha fikia baleghe.
Natija ya uhakiki huu inaonesha kuwa: Ruqayya alikuwa ni binti mchanga wa Imamu Huasein (a.s) aliyekufa muhanga karibu ya kichwa cha baba yake, pale yeye alipokuwa katika mji wa Sham, na Sukaina ni binti mwengine wa Imamu Husein (a.s), ambaye baada ya kuuliwa baba yake (a.s), yeye aliendelea kuishi kwa kipindi cha muda maalumu, kama ilivyo elezwa kwenye vitabu vya Historia.a
Wengi miongoni mwa wana-Historia pale walipokuwa wakiwazungumzia watoto wa Imamu Husein (a.s), walionekana kuwataja mabinti waliwili waliojulikana kwa majina ya Sukaina na Fatima,[1] na kuna wengine walio onekana kuongeza jina la Zainab katika nukuu zao,[2] pia kuna baadhi ya waandishi walio nukuu hali halisi ya binti mchanga wa Imamu Husein (a.s), pamoja na kuashiria hali ya huzuni ya binti huyo akiwa kwenye mji wa Sham huko Syria.[3] Wengi miongoni mwa wana-Historia na waandishi mbali mbali, wamekinukuu kisa hichi kutoka katika kitabu kijulikanacho kwa jina la (Kaamilu-Bahaai), kilichoandikwa ndani ya Karne ya saba Hijiria.
Pia ndani ya vitabu vya Riwaya na Historia vya medhehebu ya Shia, kuna dalili mbali mbali zenye kuthibitisha uhakika wa kisa hichi, na miongoni mwa maandiko yenye kuhusiana na ukweli huu, ni ibara ifuatayo:
Pale Zainabu (a.s), alipokiona kichwa cha kaka yake, hali yeye (Zainabu) akiwa katika mji wa Kufa huko Iraq, alisoma mashairi ya huzuni yenye maana ifuatayo: (Ewe ndugu yangu we! Hebu zungumza na huyu Fatima mdogo, kwani moyo wa mototo huyu unakaribia kunyongonyea na kukauka.)[4] Kauli hii ni yenye kuonesha kuwepo kwa binti huyo mchanga mwenye joto la msiba kwa kutokana na kuondokewa na baba yake.
Kwa ufafanuzi zaidi unaweza kurejea makala namba: 20076(7318)
Uhakiki wetu utakaofuata sasa, utameweza kutuonesha nukuu mbali mbali kuhusiana na kisa cha binti huyu kutoka kwa waandishi tofauti wa Kishia na Kisunni, jambo ambalo litakuwa ni lenye kututhibitishia kuwepo kwa binti huyo wa Imamu Husein (a.s) katika zama zilizopita.
Sheikh Mufiid kuhusiana na binti huyu ameandika yafuatayo: Sukaina ni miongoni mwa mabinti wa Imamu Husein (a.s), na mama yake alikuwa akijulikana kwa jina la (Rubaab).[5] Sheikh Tabarsiy naye amesema: Imamu Husein (a.s) alinuia binti huyo kumuozesha mtoto wa ndugu yake (Abdu-LLahi bin Hasan) ambaye aliuliwa katika vita vya Ashura.[6] Pia kwenye kitabu cha mashairi ya huzuni kuhusiana na msiba wa Imamu Husein (a.s), kumeandikwa maneno yafuatayo:
Yeye (Sukaina) alifunga ndoa na mtoto wa ami yake aliyeitwa Abdu-Llahi bin Hasan, na kabla ya wao kuanza maisha ya ndoa, Abdu-Llahi bin Hasan akafa muhanga katika mapambano ya siku ya Ashura, na wala wao hawakuwahi kupata mtoto katika ndoa hiyo.[7] Pia Tabarsiy amenukuu kuwa: binti wa Imamu Husein (a.s) aliyejulikana kwa jina Sukaina, yeye katika siku ya Ashura alikuwa ni mwenye umri wa miaka kumi.[8]
Mwanachuoni wa Kisunni ajulikanaye kwa jina la Dhahabiy, katika kitabu chake (Taarikhul-Islam) amesema kuwa: Sukaina ni binti wa Imamu Husein (a.s), yeye hakutosheka tu na kumuelezea binti huyu, bali pia amezitaja nukuu mbali mbali kutoka katika vitabu tofauti zenye kumzungumzia Sukaina (a.s), na idadi ya nukuu alizozitaja kuhusiana na hilo, amezitoa kutoka katika kiasi ya vitabu ishirini.[9] Pia si vitabu hivyo tu vyenye kunukuu kisa au kumtaarifisha Sukaina binti wa Imamu Husein (a.s), bali bado kuna vitabu vyengine mbali mbali ambavyo hatukuweza kuvitaja kwa kutokana na kutorefusha maneno, na kwa utafiti zaidi sisi tumekuwekea baadhi ya rejeo ambazo waweza kuzirejea kwa ajili ya kufaidika zaidi na utafiti huu.[10] Tayari hadi hapa sisi tumeshapata ufumbuzi kamili wa kumchunguza binti huyu.
Kilichobakia gizani katika utafiti huu, ni ukweli kuhusiana na umri wake, kwani sisi hatukuweza kupata kauli madhubuti kuhusiana na umri wa binti huyu, lakini vitabu mbali mbali vya Riwaya na Historia vinaonesha kuwa: pale tokeo la Karbala lilipotokea, yeye alikuwa tayari ameshaolewa, au alikuwa tayari kwa kuolewa.[11]
Paada ya sisi kuufuatilia mlolongo wa Riwaya pamoja na nukuu mbali mbali kutoka vitabuni, hapa sisi tunaweza kutoa kauli isemayo kuwa: kiancho onekana katika utafiti huu ni kwamba: Imamu Husein (a.s) alikuwa na mabinti wawili, mmoja akiwa ni Ruqayya ambaye alifariki muhanga huko Sham nchini Syria akiwa kandoni mwa kicha cha baba yake kilichokatwa huko Karbala, na mwengine ni Sukaina, ambaye alikuwa ni mwenye umri mkubwa pale tokeo la Karbala liliptokea, naye aliendelea kuishi baada ya tokeo hilo kwa muda usiofahamika sawa sawa. Na hii ndiyo natija ya mwisho tuliyo ifikia katika kukutafutia suluhu makini kuhusiana na swali lako.
Twataraji utafaidika na uhakiki wetu huu.
[1] Al-Irshaad cha Muhammad bin Nuu’maan Mufiid, mlolongo wa vitabu vya Sheikh Mufiid, juz/2, uk/135, chapa ya taasisi ya uchapishaji ya Darul-Mufiid, Beirut Lebanon, mwaka 1414 Hijiria. Manaaqibu Aalu Abi Taalib, juz/4, uk/77, taasisi ya uchapishaji ya Allaama. Aa’lamul-Waraa, cha Tabarsiy, juz/1, uk/478, taasisi ya uchapishaji ya Aalu-Bait, chapa ya kwanza, mwaka 1417 Hijiria. Nisabu Quraish, cha Mus-a’b Al-Zubairiy, uk/59, taasisi ya uchapishaji ya Darul-Maa’rif, Cairo. Ansaabul-Ashraaf, cha Balaadhiry, juz/3, uk/1288, chapa ya Darul-Fikri, Beirut Lebanon, chapa ya kwanza, mwaka 1417 Hijiria. Tadhkiratul-Khawaas, cha Sibtu bin Jouziy, uk/249, chapa ya taasisi ya Ahlul-Bait, Lebanon, chapa ya kwanza, mwaka 1401 Hijiria.
[2] Kashful-Ghumma-fi- Maa’rifatil--Aimma, cha Al-Arbiliy, juz/2, uk38, kilicho hakikiwa na Rasuliy, Tabriz, Suuq-Masjidil-Jaami-i’.
[3] Nafsul-Humuum, cha Sheikh Abbaas Qummiy, uk/415 hadi 116, chapa ya kwanza ya taasisis ya Maktabatul-Haidariyya, mwaka 1379 Shamsia. Al-Iiqaad, cha Shaa Abdul-Adhiimiy, uk/179, chini ya uhakiki wa taasisi ya Radhawiy, chapa ya kwanza ya Feiruz-Aabaadiy, mwaka 1411 Hijiria. Maa’lis-Sibtain, cha Haairiy, juz/2, uk/170, chapa ya Al-Nuu’maan, Lebanon Beirut, mwaka 1412 Hijiria. Muntahal-Aamaal, cha Sheikh Abbaas Qummiy, juz/1, uk/807, chapa ya nne ya taasisi ya uchapishaji ya Hijriy, mwaka 1411 Hijiria. Kaamilu-Bahaai, cha Imadud-Diin Tabariy, juz/2, uk/179, chapa ya Al-Mustafawiy.
[4]Bihaarul-Anwaar, cha Muhammad Baaqir Mjlisiy, juz/45, uk/115. Yanaabiul-Mawadda, cha Qanduuziy, juz/2, uk/421, chapa ya kwanza ya Sharifur-Ridhaa, mwaka 1371 Shamsia.
[5] Al-Irshaad, cha Sheikh Muhammd bin Nuu’maan Mufiid, juz/2, uk/37, chapa ya Ilmiyya Islaamiyya.
[6] Aa’laamul-Waraa, cha Tabarsiy, juz/1, uk/418, chapa ya Aalul-Bait. Al-Irshaad, cha Muhammad bin Nuu’maan Mufiid, uk/25. Kashful-Ghumma, cha Arbiliy, uk/157.
[7] Kitabu cha maobolezo juu ya kuuwawa kwa Imamu Husein (a.s), cha Abdul-Razzaaq Muusawiy, uk/397, chapa ya Basiiratiy.
[8] Rejea kitabu kilichopita.
[9] Taarikhul-Islam, cha Dahabiy, juz/7, uk/371, chapa ya Darul-Kutubil-Arabiy, Beirut Lebanon.
[10] Maqaatilit-Taalibiin, cha Abul-Faraj Isfahaniy, uk/94, 119, 133 na167. Ansaabul-Ashraafi, cha Al-Balaadhiriy, juz/3, uk/362. Al-Thuqaat, cha Ibnul- Hannaan, juz/4, uk/351, chapa ya Alkutubuth-Thaqaafa. Taariikhus-Saghiir, cha Al-Bukhaariy, juz/1, uk/273, chapa ya Daarul-Maa’rifa, Lebanon. Taariikhu Khalifatu bin Khayyaat, uk/274, chapa ya Darul-Fikri, Beirut Lebanon. Tabaqaatul-Kubraa, cha Muhammad bin Saa’ad, juz/8, uk/475, Beirut Lebanon. Tahdhiibul-Kamaal, cha Al-Mazniy, juz/6, uk/379, chapa ya Al-Risaala. Taarikhul-Madina, cha Ibnu Aa’mir, juz/2, uk/52, na juz/29, pia uk/69, chapa ya Darul-Fikri, Damascus. Ikmaalul-Kamaal, cha Ibnu Maakuulaa, juz/4, uk/316, na juz/7, uk/107, chapa ya Darul-Kutubil-Islaamiy, Cairo. Bihaarul-Anwaar, cha Muhammmad bin Baaqir Majlisiy, juz/45, uk/47 pia 169, chapa ya Lebanon. Muntahal-Aamaal, cha Sheikh Abbaas Qummiy, juz/1, uk./547, chapa ya Matbuuaa’tul-Huseiniy.
[11] Al-Irshaad, cha Muhammad bin Nuu’maan Mufiid, juz/2, uk/22, kilicho tarjumiwa na Rasuliy Mahallaatiy, chapa ya Il-Miyya-Islamiyya, rejea katika kipengele kuhusiana na wana wa Imamu Husein (a.s).